Kitabu kinachohusu Uwezeshaji wa Wanawake Tanzania kama sehemu ya Sera za Kudumisha Ustawi wa Jamii (Empowering Women in Tanzania in the Contexts of Contemporary Social Policy) kimetolewa na REPOA kwa madhumuni ya kutoa uchambuzi wa kisera, matukio na taasisi ambazo ni sehemu ya mihimili ya jitihada za serikali za kuwawezesha wanawake Tanzania. Dokezo hili linatoa muhtasari wa matokeo ya utafiti yanayoonyesha mchango wa TASAF kupitia Mpango wa Kukuza Uwezo wa Kaya Maskini katika kuwaongezea uwezo wanawake kwenye uzalishaji mali, utafutaji wa kipato, umiliki wa rasilimali na ushirikishwaji kwenye uongozi.