Kitabu hiki kina sura saba ambazo zinaangalia sera mabali mbali kuhusu maendeleo vijijini na mchango wake kwenye kupunguza umaskini Tanzania. Kinaanza na sera zilizotungwa na kuetekelezwa kipindi cha Ujamaa na Kujijetegemea. Kina sura nyingine zinazo angalia mchango wa elimu kwenye ufanisi wa kilimo;mradi wa matrekta madogo aina ya ‘power tillers’ kwenye baadhi ya wilaya; awamu tatu za sera za ruzuku za pembejeo kwa wakulima wadogo; na kilimo cha tumbaku na hatima yake kutokana na mabadiliko kwenye soko na sera za kimataifa kuhusu zao hilo. Pia kuna sura moja inayolinganisha mbinu za ukuzaji mnyororo wa thamani kwenye zao la korosho nchini Tanzania na Vietnam na nyingine ambayo inagusia mambo muhimu ya kufanikisha ushirikiano kati ya taasisi za kiserikali na asisi zisizo za kiserikali katika kutekeleza na kufanikisha sera za kilimo nchini Tanzania.