Kwenye dokezo hili tunanatoa muhstasari mfupi wa sura mbali mbali zilizopo kwenye kitabu kiitwacho ‘Youth Transition from School to Work: A Case Study of VETA in Tanzania (Kipindi cha Mpito kwa Vijana Kati ya Mafunzo na Ajira: Mchango wa VETA Tanzania), chenye lengo la kuongeza uelewa wa matatizo wanayopitia vijana kwenye jitihada zao za kutafuta ajira baada ya mafunzo. Nia ni kutafuta njia ya kuwapunguzia vikwazo hivyo na kuongeza mchango wao kwenye jitihada za taifa za kujenga uchumi unaoongozwa na Viwanda. . Kwenye dokezo hili tunaangalia mambo gani yanawasaidia au kuwapunguzia vijana uwezo wa kupata ajira mara tu baada ya mafunzo, hasa kuhusu jinsi wanavyotayarishwa kuingia kwenye ulimwengu wa kazi, matarajio yao ukiyalinganisha na hali halisi kwenye soko la ajira na uhusiano ulioko kati ya kazi zilizopo, taarifa kusu hizo kazi, stadi wanazokuwa nazo na viwango vyao vya elimu.
Publisher : REPOA
Download .PDF